MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAFUTA AJIRA

Ijumaa, Oktoba 21, 2016 Christian Bwaya Mambo Sita ya Kufanya Unapotafuta Kazi Kutafuta kazi ni kuingia kwenye soko la ajira ambalo kimsingi ni uwanja unaowakutanisha watu wenye mahitaji makubwa ya aina mbili. Upande mmoja, wapo watu wenye ‘bidhaa’ ya ujuzi na weledi, lakini wenye hitaji la kujipatia kipato kwa kutumia ujuzi na maarifa waliyonayo. Hawa wanaitwa watafuta kazi. Upande wa pili, wapo watu wenye uhitaji wa ujuzi huo ili uwasaidie kuongeza ufanisi wa huduma wanazotoa kwa kutumia raslimali na fedha za kuulipia ujuzi huo. Hawa wanaitwa waajiri. Pande hizi mbili zinahitajiana na kutegemeana kwa maana ya hitaji la upande mmoja hufanyika jawabu la upande wa pili. Ili uweze kuajirika, unalazimika kumridhisha mwajiri kuwa unao ujuzi na uwezo wa kutumia maarifa uliyonayo katika kuongeza ufanisi wa huduma anazozitoa. Kutokana na ukweli kwamba waajiriwa hutofautiana ujuzi na uwezo huo, na kwa sababu uwezo wa waajiri kadhalika hutofautiana, na kwa kuwa haiwezekani kila ...