WALIOFAULU USAILI WA AJIRA SERIKALINI KUFUTWA

Watu wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa, watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo zitakapotangazwa tena. Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Hilo limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa. Taarifa hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa. "Kwa mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vy...