Hapa Kazi Tu
BREAKIN NEWZZ!!;- RAIS MAGUFULI ATUMBUA JIPU LINGINE SASA HIVI SOMA HABARI KAMILI HAPA LIVE!!

Rais John Pombe Magufuli ameagiza kuwa Wakurugenzi wote wa Wizara mbalimbali watakaohudhuria vikao vya kamati za bunge Mjini Dodoma, watasafiri kwa mabasi badala ya magari yao "mashangingi" ya serikali kama ilivyozoeleka.
Katika utaratibu huo mpya kila Wizara itakodi basi (Coaster) kwa ajili ya kusafirisha Wakurugenzi hao kwenda Dodoma kwenye vikao vya bunge ili kutoa msaada kwa wizara zao pale wanapohitajika kufanya hivyo. Rais amefikia maamuzi haya ktk jitihada za kupunguza gharama za mafuta na posho za madereva wa wakurugenzi wanaposafiri kuelekea Dodoma.
Hata hivyo Wakurugenzi hao hawazuiwi kusafiri kwa magari yao binafsi (personal) kwa kujilipia gharama zote wao wenyewe ikiwa watataka kufanya hivyo. Katika utaratibu huu mpya inamaanisha kuwa viongozi wa wizara watakaosafiri kwa "mashangingi" kuelekea Dodoma ni Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu mkuu tu.
Source: Kurugenzi ya Habari Ofisi ya Rais.!
Maoni
Chapisha Maoni